Vigogo Afrika Wagombea Saini ya Fei Toto




KUFUATIA kuwepo kwa taarifa ya klabu kubwa za Afrika kuwa kwenye mchakato wa kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’, uongozi wa klabu hiyo umeweka wazi kuwa upo tayari kumwachia nyota huyo kama watapokea ofa nono.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa mpaka sasa baadhi ya klabu kubwa kama Orlando Pirates, Al Masry na TP Mazembe zimeonyesha nia ya kuwasilisha ofa ya kumsajili kiungo huyo mara tu baada ya dirisha kubwa la usajili kufunguliwa.

Kuendana na mtandao wa Transfer Market ambao unajihusisha na tathmini ya thamani za wachezaji, Fei Toto kwa sasa ana thamani ya zaidi ya euro 75,000 ambazo ni sawa na zaidi ya Sh milioni 195 za Kitanzania.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mwenyekiti wa Kamati ya ufundi ya Yanga, Dominic Albinus alisema: “Tumekuwa tukisikia kuhusu taarifa za mchezaji wetu Feisal Salum kutakiwa na baadhi ya timu za nje, lakini nikuweke wazi kuwa mpaka sasa hakuna ofa yoyote rasmi ambayo imefika mezani kwa ajili yake.

“Lakini msimamo wetu juu ya suala hilo na uhamisho wa wachezaji kiujumla ni kwamba tuko tayari kumruhusu mchezaji yeyote ikiwa tu makubaliano yatafikiwa.

“Kuhusu thamani yake hilo linatokana na urefu wa mkataba wake, ambapo kwa Feisal bado ana mkataba zaidi ya miaka mitatu hivyo kwa kuongeza na kiwango chake uwanjani lazima klabu ipate ofa ya maana ili kumuachia.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad