Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune ametangaza kuwa kuanzia March mwaka huu wa 2022, Serikali yake itaanzisha mafao ya ukosefu wa ajira kwa vijana kwa lengo la kulinda utu wa vijana.
Kila Kijana asiye na ajira katika Taifa hili linalokadiriwa kuwa na Watu milioni 45 atapata dinari 13,000 ambazo ni sawa na USD 92 na sawa na Tsh. 213,000 ambapo malipo yataendelea mpaka Mhusika atakapopata kazi.
Malipo haya ya kila mwezi yataambatana na huduma nyingine kama vile matibabu bure huku kodi kadhaa katika baadhi ya bidhaa za walaji zikiondolewa kutoka kwenye malipo hayo ambayo ni sehemu ya bajeti ya mwaka 2022.
Taifa hilo la Afrika Kaskazini linapambana na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira kwa karibu 15% pamoja na kwamba Nchi hii ni muuzaji mkubwa wa gesi Barani Afrika ambapo asilimia 90 ya mapato yake yanatokana na mafuta na gesi. #MillardAyoUPDATES