Waamuzi waliochezesha Simba, Yanga wapewa adhabu




Mwamuzi Ahmada Simba aliyechezesha mchezo wa Simba SC na Tanzania Prisons na Mwamuzi Hussein Athumani aliyechezesha mchezo wa Yanga dhidi ya Mbeya City wameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizunguko mitatu kwa kushindwa kutafsiri sheria kwenye michezo ya Ligi kuu Tanzania bara.
Waamuzi hao wameondolewa kwenye orodha kufuatia kikao cha kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Ligi kuu Tanzania bara TPLB katika kikao chake cha Februari 10, 2022 kilichopitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi.

Mwamuzi wa kati wa mchezo namba 109 kati ya Yanga dhidi ya Mbeya City ambao ulimalizika kwa suluhu (0-0), Husseina Athumani kutoka Katavi  na mwamuzi msaidizi namba mbili godfrey Msakila wamkoani Geita wameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizunguko mitatu kwa kosa la kushindwa kutafsiri vema sheria za mpira wa miguu katika mchezo huo uliochezwa Februari 5, 2022. Hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 42 ya Ligi Kuu Kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi.

Kwenye mchezo huu Mwamuzi msaidizi namba 2 Godfrey Msakila alitafsiri moja ya tukio kuwa mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele alikuwa kwenye nafasi ya kuotea na kumnyima nafasi ya kufunga kwenye mchezo huo ambao ulimalizika kwa suluhu.

Mwamuzi Ahmada Simba kutoka Kagera ambaye alichezesha mchezo namba 112 wa ligi Kuu kati ya Simba dhidi ya Tanzania Prisons ambao ulimalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0, naye ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi kwa mizunguko mitatu kwa kosa la kushindwa kutafsiri sheria za mpira wa miguu katika mchezo huo uliochezwa Februari 3, 2022.


 
Katika mchezo huo mwamuzi Ahmada Simba aliwapa penati Simba SC kwa kile kilichoaminika kuwa kuna mchezaji wa Prisons aliushika mpira wakati simba wakiwa wanashambulia ingawa picha za marudio za Televisheni zilionyesha kuwa hakuna mchezaji ambaye alishika.

Kwa upande mwingine klabu ya yanga imepigwa faini ya shilinhi Milioni moja kwa kosa la mashabiki wake kuwarushia chupa za maji waamuzi kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City. Lakini pia mchezaji wa timu hiyo Dickson Job amefungiwa michezo 3 na faini ya shilingi laki tano kwa kosa la kumkanyaga kwenye mbavu mchezaji wa Mbeya City, Richard Ng'odya jambo lillilotafsiriwa kuwa ni mchezo wa hatari.

Na Afisa Habari na mawasiliano wa klabu ya Yanga Hassan Bumbuli na Haji Manara wametozwa faini ya shilingi Laki tano kila mmoja kwa kosa la kuwashutumu waamuzi wa Ligi Kuu NBC kupitia Vyombo vya Habari

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad