Jeshi la taifa la Kongo FARDC limetangaza kuwakamata raia watatu wa Tanzania ambao ni waasi wa ADF waliosajiriwa wilayani Beni mashariki mwa Kongo.
Raia hao wa Tanzania, walikamatwa Jumapili hii, Februari 6, 2022 wakati wa doria zilizofanywa na askari wa Kongo katika bonde la Mwalika, katika eneo la Beni Kivu Kaskazini.
Kulingana na taarifa ya msemaji wa secteur (tarafa) ya Sokola 1 Kivu Kaskazini, Kapteni Athony Mwalushayi ; waasi hao wamekiri kuwa walisajiriwa kwa nia mbaya na raia wa Kongo ambaye aliwadanganya kwamba watafanya kazi katika migodi ya dhahabu, lakini wakajikuta katika kikundi cha waasi wa ADF.
Akizungumza na BBC, Kapteni Athony Mwalushayi amesema, waasi hao raia wa Tanzania wako sasa mikononi mwa idara husika ili waandelee kuchunguzwa.
Mnamo Januari 28, katika eneo hilo hilo la Beni, FARDC pia lilimkamata muasi wa ADF, raia wa Kenya, Salim Muhammad, ambaye alikuwa anasambaza video za ukatili.
Januari 9, 2022, Benjamin Kisokeranio, mkuu wa tawi la ADF la muasi Jamil Mukulu, alikamatwa Uvira katika jimbo la Kivu Kusini