Wataalamu kutoka NIT, Taasisi ya Karolinska na MUHAS wanasema wanaovuka Barabara huhatarisha Maisha yao kwa kutotumia Madaraja ya juu yaliyopo baadhi ya maeneo kama Buguruni, Manzese, Morocco, Kimara na Ubungo
Sababu ya kukwepa Madaraja hao imetajwa kuwa ni urefu wa Madaraja na Watu kuhofia Wizi na Uporaji. Hali hiyo imetajwa kuwa changamoto kwa kuwa 30% ya Ajali zinazotokea Nchini zinahusisha watembea kwa Miguu ambao wangepunguza hatari kwa kutumia Madaraja yaliyopo
Wataalamu wameshauri kuwepo na ushirikishwaji wa Wananchi kabla ya Ujenzi wa Madaraja ambayo hayatumiwi ipasavyo.