Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limewakamata Watu 17 kwa tuhuma za kuuza jezi bandia za Timu ya Yanga Afrika zinazotengenezwa na kusambazwa na kampuni ya GSM.
Kazi hiyo ilifanyika katika maeneo mbalimbali ya Jiji Dar es salaam lakini pia kwa kushirikiana na baadhi ya mikoa nchini kwa kipindi cha kuanzia tarehe 02.01.2022 hadi tarehe 28.01.2022.
Katika Jiji la Dar es salaam Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa watano, akiwemo Zahiri Hassan (17) Mmwera aliyekutwa huko Uwanja Benjamin William Mkapa akiwa na Jezi bandia za Timu ya Yanga 52, Kariakoo Mtaa wa Agrey alikamatwa Majiba Ndahya (50) akiwa na Jezi 124, Mohamed Ramadhani (26) alikutwa na Jezi 86, John Staslaus (19) alikamatwa na Jezi 39 na Emmanuel Kinasa (21) alikutwa na Jezi 60.
33
Watuhumiwa hao waliwataja wenzao wa Zanzibar, ambapo Uwanja wa Amani watuhumiwa watatu walikutwa na Jezi bandia 36, jezi nyingine bandia 134 zilipatikana kwa kushirikiana na Polisi Mkoa wa Tanga na Mwanza ambapo watuhumiwa tisa walikutwa na Jezi 811.
"Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linawatahadharisha wananchi wote wanaojihusisha na vitendo vya kutengeneza, kuuza na kusambaza, bidhaa kwa kuiga au kufananisha nembo za biashara au huduma za watu wengine iliyosajiliwa kisheria, kufanya hivyo ni kosa na kinyume na sheria za nchi"