KUELEKEA mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi raia wa Tunisia, ameamua kumbadilishia mbinu mshambuliaji wake, Fiston Mayele kuhakikisha hakwami katika suala la kufunga mabao.
Mayele mwenye mabao sita na asisti mbili kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu, anatarajiwa kuanza kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Februari 23 mwaka huu.
Chanzo chetu kutoka Yanga, kimeeleza kwamba: “Kwa mazoezi ya jana (juzi Ijumaa) kocha nimemuona akimfundisha Mayele mbinu mpya akiongeza , hii ni baada ya kuamua kuongeza idadi ya viungo kuelekea mechi dhidi ya Mtibwa.
“Kama unavyofahamu kwenye mechi zilizopita mara nyingi katika safu ya ushambuliaji, Mayele alikuwa akisaidiwa na Saido (Saidi Ntibazonkiza), Zakini katika mechi hii, kuna uwezekano Saido asicheze.“Kwenye viungo nimeona anaweza kuanza na Fei Toto, Bangala na Aucho, sababu kubwa ni kwenda sawa na Uwanja wa Manungu ambao bado haujawa kwenye ubora katika sehemu ya kuchezea.”