WAKAZI amchana MRISHO MPOTO "Nitakunyoa hiyo RASTA na chupa, ukisikia jina langu kaa mbali"
Ameandika haya Wakazi"
MRISHO ARISTOTEE MPOTO
Mjomba naona anataka kuwa kama Aristotee! Kuropoka tu ilimradi mdomo mali yako…. Kama hujaelewa Wakazi alimaanisha nini, ni bora ukae kimya au umuulize anayekuhoji vizuri.
Kama msanii unapaswa kuwa responsible hasa pale ambapo kuna media mbele yako. Eti Wakazi ananongwa?! IPI HIYO?!
Wasanii walioalikwa ni wachache, fomu ya alphabetic order imemuweka mmoja juu nje ya order, na pia kuna wasanii wamefariki wapo kwenye list! Event inawahusu wasanii wote na sio tu ya Mirabaha bali pia Tuzo. HIZI NI FACTS!!
FACT nyingine ni kwamba kuna wasanii imezoeleka kuwa huwa hawaalikwi kabisa, na ndio hao hao walioamini na kuendelea kuamini kuwa issue ni ya kimichongo na wao hawahusiki maana hawahusishwi.
JIBU LA MPOTO: Wote wamealikwa (Uongo mtupu; kuna watu walikuja wakazuiwa kuingia)
JIBU LA BASATA: Tulihusisha Vyama husika na Shirikisho.
JIBU LA SHIRIKISHO: Tulihoji nakuambiwa tuna nafasi chache hivyo tutaita wale waliojiandikisha Cosota tu! (kikao hakikuwa cha Cosota tu bali Basata pia na agenda zilikuwa mbili MIRABAHA NA TUZO)
Sasa ndugu Mpoto nongwa yangu iko wapi, wakati hata majibu yenu tu baada ya sisi kuhoji YANAPISHANA?!
Alafu for the record, mimi sihitaji vimialiko vyenu… Ila nachohoji na cha msingi, je utawezaje kuwavutia hao Wasanii ambao hawajajiandikisha Cosota na Basata kuja, kama utaendelea kuwatenga kwenye shughuli ambazo pengine wangekuja kuona na kutambua UMUHIMU WAKE?! Kuna watu wamepaza sauti na kupambania haya mambo ya wasanii kulipwa Mirabaha na wao hawajaalikwa vile vile badala yake mnatuwekea wasanii wenu mnaotaka na hadi walitangulia mbele za haki.
Tanzania tunachelewa sana kimaendeleo sababu ya kuweka mbele siasa. Na cha ajabu siasa zenyewe sasa hivi zina-adapt INCLUSION.
Mwambieni Mpoto akitajiwa jina langu aachane nalo, nakuja kumnyoa rasta zile kwa chupa! " Wakazi