Kilio cha baadhi yenu ni kwa nini sijaenda Private kuwaelekeza. Kwamba wafanye kitu PUBLIC alafu mimi nitoe maoni in PRIVATE… Sawa good suggestion!
Ila ikumbukwe kuwa Wao sio wa kwanza kufanya makosa ya namna hii, na pia sio wa kwanza kwa sisi kuwasema hadharani tena kwa kushauri na sio kuwa zodoa wala kukejeli.
2017: Q Boy Msafi alivaa Mavazi ya Ku Klux Klan (Kundi ya kibaguzi la Marekani) na pia nguo zenye Nembo ya Swastika (Ya Hitler wa Ujerumani) kwenye video yake na tukamsema HADHARANI.
2019: Mr Blue alitoa video amevaa Gestupo Uniform na Nembo ya Swastika pia (Uniform za Police wa Nazi) na yeye tukamsema HADHARANI.
2021: TCRA waliwafungia Wasafi Media miezi 6 kwa ile issue ya Gigy Money (ambae nae alionewa) na sisi tukapaza sauti kuwatetea Wasafi HADHARANI.
So moja, sisi hatuna kinyogo nao, na wakionewa huwa tupo nao, na hatuna hila wala kisasi wa wivu. Mbili, pengine Dai angejifunza kutoka kwa hao ambao walifanya mistakes hizo akahakikisha harudii same mistakes. Wasanii wa TZ kwa makosa tunayofanyaga kwenye videos na picha zetu huwa yanafanya tuonekane shallow sana nje huko. Na ni vyema kuweka mapungufu haya hadharani ili tuwasaidie Wasanii wa kizazi kijacho! Mbali na yote, wananchi wamefurahia kufahamu kidogo historia. Sio mbaya!! " Wakazi