Waliosambaza nyaraka za serikali kutafutwa



Mkuu wa wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Toba Nguvilla, amemwagiza mkuu wa polisi wilayani humo kufanya uchunguzi wa kubaini waliohusika kusambaza mitandaoni barua ya kuhamisha fedha shilingi mililioni 470 kutoka akaunti ya shule ya sekondari Ikondo kwenda shule ya sekondari Karambi.

Agizo hilo amelitoa katika kikao cha baraza la madiwani wa halmshauri ya wilaya hiyo, cha kujadili taarifa ya robo ya pili ya mwaka inayoanzia Oktoba hadi Desemba 2021, baada ya kubaini kuwa kuna baadhi ya watu wamesambaza mtandaoni barua hiyo amabayo ni nyaraka ya serikali

Akitoa ufafanuzi kwa niaba ya Mkurugenzi, Afisa Elimu Sekondari wa halmashauri hiyo, Jared Muhile, amesema halmashauri iliweka mipango ya kujenga shule mpya tatu za sekondari, chini ya mpango wa kuendeleza shule za sekondari, ambazo ni Mafumbo, Mushabago na Kamishango, kwa lengo la kuwapunguzia wanafunzi tatizo la kutembea umbali mrefu kwenda shule.

Amesema kuwa baada ya kuanisha shule hizo ambazo fedha zake ni kutoka serikali kuu, baadaye Katibu Mkuu wa TAMISEMI alituma maelekezo kwamba fedha ambazo ilikuwa zijenge shule shikizi ya sekondari Kamishango zinahamishwa na kwenda kujenga shule ya sekondari Karambi, maamuzi ambayo ambayo baadhi ya wananchi na viongozi wa kata hiyo hawakuridhishwa nayo.


 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad