Wasira "Sitaki Tena Uraisi"



MBUNGE wa zamani na Waziri Mstaafu wa Wizara mbalimbali nchini, Mzee Steven Wasira amesema kuwa kwa sasa hana mpango tena wa kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na umri kumtupa mkono huku akiwataka wale wanaonyemelea kiti hicho mwaka 2025 kumwachia Rais Samia Suluhu amalize miaka yake 10.

Wasira amesema hayo leo Jumatatu, Fabruari 7, 2022 wakati akiwasalimia wananchi wa Bunda na kutoa shukrani kwa Rais Samia ambaye alikuwa ziarani mkoani Mara.

“Nitumie nafasi hii kama Mtu mzima na Kiongozi wa siku nyingi katika Mkoa wa Mara kukupongeza Rais Samia na kukuhakikishia kwamba Wananchi wa Mara kwa kazi unayofanya wanakuunga mkono kabisa.

“Na wale wanaosema wanautaka Urais mwaka 2025 Mimi nawashauri wasubiri kwa sababu kwa utamaduni wa CCM kama una Rais aliyopo Ofisini huwa hatumpingi tunampa nafasi amalize kipindi cha awamu hiyo ambayo huchukua miaka 10.

“Kama una umri mkubwa na unafikiri ikipita miaka tisa utazeeka basi acha kwasababu hatuwezi kuwa Marais wote, Mimi niliutaka Urais sasa hivi siutaki tena kwasababu umeshanipita sasa wanakuja wengine, sasa kama na wewe una miaka mingi na una mashaka kama usipoupata mwaka 2025 utachelewa ni bahati mbaya,” asema Mzee Wasira.

Wasiara mwenye umri wa miaka 77 sasa, aliwahi kuomba ridhaa ndani ya chama chake cha CCM kuwania urais mwaka 2015 hakufanikiwa na badala yake alipitishwa Dkt. John Pombe Maguduli ambaye alikuja kushinda urais na kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad