Waziri wa Ukraine Atangaza vifo vya Raia 137 na Majeruhi 169


Waziri wa Afya wa Ukraine, Viktor Lyashko ametangaza vifo vya raia 137 na majeruhi 169 ndani ya siku moja tangu nchi hiyo ivamiwe na Urusi. Watu 57 katika ya 137 waliopoteza maisha ni wananchi wa kawaida na kundi lililobaki ni wanajeshi wa Ukraine.


Picha hii inaonyesha hatua ya Urusi kuvamia Ukraine ilivyoathiri usafiri wa angani barani Ulaya huku mashirika ya ndege yakiepuka anga ya Ukraine wakati mzozo wake na Urusi ukizidi kufukuta.

Ukraine ilifunga anga yake kwa safari za ndege za kiraia saa za mapema baada ya Urusi kuanza mashambulizi yake.

Waziri wa Uchukuzi wa Uingereza Grant Shapps ameagiza Mamlaka ya Usafiri wa Anga kuhakikisha mashirika ya ndege yanaepuka anga ya Ukraine “kufuatia matukio ya kutisha usiku mmoja”.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad