Wema Sepetu "Sasa Nina Amani ya Moyo"



WEMA Isaac Sepetu; ni supastaa asiyechuja wa Bongo Movies ambaye anafunguka kuwa, miongoni mwa vitu ambavyo anajivunia kwa sasa ni kuwa na amani ya kutosha ndani ya moyo wake.

Wema anasema hana kingine zaidi maana hicho ndicho kitu pekee ambacho kinampa nguvu ya kusonga na maisha bila kokoro.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Wema ambaye kwa sasa mashabiki wake wanapenda kumuita Last Born wa Taifa; yaani Kitindamimba au Kiziwanda wa Taifa), anasema kuwa, kwa sasa hakuna mtu wa kumkosesha raha au kumkera kwa namna yoyote.

Wema anasema anachoshukuru ni kwamba ana amani kubwa ndani ya moyo wake na si kitu kingine kama watu wanavyomfikiria. Mrembo huyo mwenye nyota zake anasema amejikuta kwenye hali hiyo baada ya kujitambua vilivyo na akaona wazi silaha kubwa ni kuwa na amani ndani ya moyo.


“Unapokuwa na amani ndani ya moyo wako kama nilivyo kwa sasa, huwezi kuamini ni kitu kikubwa sana na kitaweza kukulinda mno katika maisha yako, lakini kama huna amani, unaweza kufa hata kwa msongo wa mawazo tu,” anasema Wema ambaye hivi karibuni alichokozwa na mtu anayejiita Aristote ambapo jeshi lake lilimtetea kwa nguvu zote.

STORI; IMELDA MTEMA, DAR

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad