Wizara ya Uchukuzi Yaanika Sababu za Hasara ATCL



Dar es Salaam. Siku chache baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuwasilisha bungeni taarifa yake ya utekelezaji wa shughuli kwa mwaka 2021/2022 ilieleza kuwa Shirika la Ndege la Tanzania limepata hasara jumuishi ya Sh152.96 bilioni tangu mwaka 2015/16.

Leo Jumatano, Februari 23, 2022 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya Uchukuzi), Dk Ally Possi alitembelea ofisi za ATCL zilizopo jijini Dar es Salaam na kuweka wazi kuwa athari za ugonjwa wa Uviko-19 ni chanzo cha hasara ya Sh60.24bilioni katika shirika hilo.

Akijibu swali mbele ya wanahabari leo wakati wa ziara yake ofisi za ATCL, Dk Possi amesema;

“Hasara ile imetengenezwa na sababu nyingi, kama utakumbuka ugonjwa wa Uviko ulikuwa umeathiri sekta ya usafirishaji wa anga sio kwetu tu ila mashirika mengi ya ndege duniani tukiwamo sisi pia,”amesema.


Hata hivyo amesema kumekuwa na juhudi za kukabiliana na hasara hiyo ikiwemo kuboresha viwanja vya ndege nchini huku Serikali ikijiandaa kupokea ndege nyingine tano ilizonunua ili kukuza mapato

Kwa mujibu wa ATCL, kwa sasa ina jumla ya vituo 15 vya safari ndani ya nchi na vituo vinane nje huku ikiingia ushirikiano wa huduma za usafiri na mashirika ya ndege ya Rwanda, Qatar, Ethiopia.

Kuhusu fursa ya usafirishaji wa bidhaa za ndani katika masoko ya nje, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Ladislaus Matindi amesema tayari wameshaanza kuifuatilia fursa hiyo kwa masoko ya India na Marekani

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad