Yanga Waanza Kiburi...Wavimba na Point Tano Walizowapita Simba



MABINGWA mara 27 wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wameweka wazi kuwa pointi 5 ambazo wamewapita wapinzani wao Simba ni nyingi na zinawapa nguvu ya kuweza kutwaa ubingwa.

Yanga wanaongoza ligi wakiwa na pointi 36 baada ya kucheza mechi 14 huku mabingwa watetezi Simba wakiwa na pointi 31 baada ya mechi 15, tofauti ya pointi tano na Yanga ambao wana mchezo mmoja mkononi.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Mkuu wa Kitengo cha Habari ndani ya Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa pointi tano walizonazo kibindoni sio chache zinawapa hali ya kujiamini na nguvu ya kutwaa ubingwa.

“Tunaongoza ligi ipo wazi na tumewaacha wapinzani wetu kwa tofauti ya pointi tano, hizo sio za kubeza zinatupa nguvu ya kuweza kusaka ubingwa wa ligi na tunahitaji kuweza kutwaa kwa kuwa tumejipanga.

“Wachezaji wapo tayari na benchi la ufundi linaendelea kuwapa mbinu wachezaji, mapumziko yamekwisha kila mmoja kwa sasa yupo kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu ujao na haitakuwa kazi rahisi kupata ushindi lakini tupo tayari kwa ajili ya kupata matokeo,” alisema Bumbuli.

Mchezo ujao wa Yanga kwenye ligi ni dhidi ya Mtibwa Sugar unatarajiwa kuchezwa Februari 23, Uwanja wa Manungu, Morogoro.

Marco Mzumbe, Dar es Salaam
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad