Yanga Washtukia, Wamuonya Mayele



MABOSI wa Yanga ni kama wameshtukia vile, unaambiwa juzi walimuita straika wao Fiston Mayele kufanya naye kikao na kumuonya kuhusu suala la kuzungumza na waamuzi pamoja na kupunguza jazba kila anapokuwepo uwanjani.


Hiyo ni kutokana hofu ya kutafutiwa kadi za makusudi zitakazomsababishia kufungiwa na kuikosa michezo muhimu ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) msimu huu.


Mayele, mwenye mabao sita, anachuana vikali katika ufungaji bora na mshambuliaji wa Namungo FC, Reliants Lusajo aliyefunga tisa.


Mmoja wa mabosi wa Yanga, ameliambia Championi Ijumaa kuwa adhabu ya beki wa pembeni Mkongomani, Shaaban Djuma ndiyo imeshitusha na kufanya naye kikao kwa hofu ya yeye kukutana na adhabu hiyo wakati yeye ndiye mshambuliaji tegemeo.


 

Bosi huyo alisema kuwa wameshitukia mabeki wa timu pinzani kuwapania washambuliaji wao na kuwachezea rafu za makusudi kwa lengo la kuwakasirisha halafu warudishie ili wapewe kadi na kufungiwa kama ilivyotokea kwa Djuma.


Aliongeza kuwa mshambuliaji huyo ameshauriwa kupunguza jazba na kuwapuuza mabeki wa timu pinzani wenye lengo la kumtoa mchezoni kwa kumchezea vibaya.


“Mayele mwenyewe uzuri ameshajua kila kitu kinachoendelea juu ya mabeki wa timu pinzani wenye lengo la kumtoa mchezoni kwa kumchezea rafu za makusudi huku wakitumia nguvu nyingi katika kumkaba.



“Hivyo kutokana na umuhimu wake, Mayele katika timu anapokuwepo uwanjani, haraka uongozi umemuita kwa ajili ya kufanya naye kikao kizito.


“Katika kikao hicho pia walikuwepo baadhi ya wachezaji tegemeo katika timu ambao wanapaniwa kila wanapokuwepo uwanjani na wachezaji wa timu pinzani,” alisema bosi huyo.


Akizungumzia hilo, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alisema: “Tunafahamu kila kitu kuhusiana na hujuma zinazofanywa na wachezaji wa timu pinzani zenye lengo la kuwatoa mchezoni wachezaji wetu.


“Wachezaji wetu wanachezewa rafu za makusudi kutokana na kupaniwa na wanafanya hivyo kwa lengo la kutaka kulipiziwa pale wanapowachezea wachezaji wetu kama ilivyotokea kwa Djuma, hivyo tayari tumewaonya wachezaji wetu.”


 

Mayele naye hivi karibuni aliwahi kusema: “Mabeki wa timu pinzani walishaniona mimi ndiyo tishio katika timu, hivyo wanacheza kwa kutumia nguvu nyingi kila ninapokuwa nina mpira.


“Tayari nimeongea na kocha wangu Nabi (Nasreddine) kwa ajili ya kuniongezea mazoezi ya binafsi ya nguvu ili nitakapokutana nao niweze kupambana nao
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad