Young Africans Hawa si Mchezo, Kuvunja Rekodi ya Simba SC Kimataifa

 


Uongozi wa Young Africans umeweka malengo ya kuiweka klabu hiyo kwenye nafasi 10 bora Barani Afrika, endapo itapata nafasi ya kushiriki Michuano ya Kimataifa msimu ujao 2022/23.


Young Africans imedhamiria kuiwakilisha Tanzania kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, ikiwa kama Bingwa wa nchi, kufuatia mipango na mikakati waliojiwekea msimu huu 2021/22.


Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Fredrick Mwakalebela amesema, wamedhamiria kuifikisha pazuri klabu hiyo, baada ya kuwa mabingwa wa Tanzania Bara msimu huu, na wanaamini hilo linawezekana.


Amesema klabu yao ina nafasi kubwa ya kuiweka pazuri Tanzania kimataifa, huku wakiamini hilo litawezekana endapo watafanikiwa kucheza Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu ujao.


“Sasa tunataka tuwe katika nafasi 10 bora Afrika, huko chini tumeshavuka. Watanzania bila kujali ushabiki tuendelee kuiombea Young Africans ili izidi kufanya vizuri kwa msimu ujao tutaibebe nchi kimataifa na malengo yetu ni kuhakikisha tumeingia katika vilabu 10 Bora Afrika”. amesema Mwakalebela


Msimu huu 2021/22 Young Africans ilishiriki Ligi ya Mabingwa Barani Afrika hatua ya awali, lakini ilitolewa kwa kufungwa jumla ya mabao 2-0 na Rivers United ya Nigeria.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad