Young Africans yalalamikia waamuzi Ligi Kuu



Uongozi wa klabu ya Young Africans umepaza sauti na kusema timu yao imekua ikipata wakati mgumu dhidi ya waamuzi wanaochezesha michezo yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Young Africans imetoa kauli hiyo kupitia Idara ya Habari na Mawasilino inayoongozwa na Hassan Bumbuli kwa kutumia Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Jumanne (Februari 08), jijini Dar es salaam.

Bumbuli amesema: Tunaongoza Ligi kwa tofauti ya alama 5, pamoja na hayo yote tunapenda kueleza kwamba haturidhishwi na mwenendo wa baadhi ya waamuzi wanaochezesha michezo yetu ya Ligi Kuu.”

“Hii imetokana na mlolongo wa matukio ya maamuzi yenye utata dhidi ya timu yatu.”


 
Mwishoni mwa juma lililopita Young Africans ilipata wakati mgumu dhidi ya Mbeya City FC kwa kulazimishwa sare ya bila kufungana, huku madai ya baadhi ya wanachama na mashabiki wao wakisisitiza mwamuzi aliinyonga timu yao kwa shambulio na Mayele kuzimwa kwa kigezo cha kuotea. Young Africans inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania ikiwa na alama 36, ikifuatiwa na Mabingwa watetezi Simba SC yenye alama 31.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad