Zari Hassan Ashindwa Kumzima Zuchu..Atafuta Kutrend Kwa Nguvu na Kiben 10



BABY mama wa msanii mkubwa nchini Tanzania, Nasibu Abdul au Diamond Platnumz, mwanamama Zarinah
Hassan ‘Zari The Boss Lady’, anadaiwa kushindwa kuhimili kishindo cha tetesi za jamaa huyo kutoka kimapenzi na msanii wake, Zuhura Othman ‘Zuchu’, IJUMAA linaripoti.

Kwa wiki kadhaa sasa, kumekuwa na uvumi kwamba, huwenda Zuchu akavishwa pete ya uchumba na Diamond kutokana na kushamiri kwa penzi lao na kama kuna mtu anabisha kuwa si wapenzi, basi akae hivyohivyo.

ASHINDWA KUZIMA MOTO
Penzi la Diamond au Mondi na Zuchu linadaiwa kumfanya Zari kuhaha na kujikuta naye akitafuta kutrendi kwa nguvu zote na mwanaume anayesemekana ni mpenzi wake mpya, lengo likiwa ni kuzima moto wa Mondi na Zuchu, lakini amejikuta akishindwa vibaya.


Zari ameendelea kuibua gumzo wakati huu baada ya kumuanika mwanaume huyo ambaye amekuwa akijiachia naye huku kukiwa na madai yaleyale kwamba naye ni mdogo kiumri (kiben’teni).



Picha za kumwaga za kimahaba zimefanya baadhi ya wafuasi wake kuamini kwamba Zari yupo kwenye mahaba mazito na jamaa huyo.

Watu wa karibu na Zari wanasema kuwa, habari za Diamond kutaka kumuoa Zuchu zimemvuruga kabisa na kujikuta akitafuta mwanaume wa kumpunguzia mawazo juu ya wawili hao.

MWANAUME AJULIKANA
Uchunguzi wa Gazeti la IJUMAA umebaini kwamba, mwanaume huyo ni raia wa nchini Uganda ambaye anafahamika kwa jina maarufu la GK Choppa ambaye anatajwa kuwa na pesa za kumwaga.


Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uganda, GK ndiye aliyempokea Zari alipokwenda kuishi Durban nchini Afrika Kusini ambapo wamekuwa wakionekana pamoja wakila bata za kutisha hadi kuku wanaona
wivu.


Hata hivyo, Zari amekuwa akitumia nguvu kubwa kukanusha kwamba, yeye na GK ni wapenzi, lakini matendo yao yanaakisi mahaba yao. Kwa mfano; lipo tukio la video inayomuonesha Zari akimhudumia mwanaume huyo
chai au uji kwa kupiga magoti kama wafanyavyo baadhi ya jamii za nchini Uganda pale mwanamke anapomhudumia mumewe hulazimika kupiga magoti.


HUYU HAPA ZARI
Kupitia kituo kimoja cha habari cha nchini Uganda, Zari anaeleza kuwa, jamaa huyo ni rafiki yake na si mpenzi wake kama wanamtandao wanavyodhani.

“Ni rafiki yangu huyu, tafadhali acheni kueneza uongo mtandaoni,” anasema Zari. Zari ambaye amezaa watoto
wawili na Diamond, tangu waachane amekuwa akidaiwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi mara tu kunapokuwa
na tetesi za Diamond naye kuingia kwenye penzi jipya, lakini baada ya tetesi hizo kumalizika naye husemekana ameachana na mwanaume husika.


MOTO WA DIAMOND NA ZUCHU
Pamoja na hayo yote anayoyafanya Zari, lakini moto wa fununu za muda mrefu katika mitandao ya kijamii huku zikipambwa na picha za matukio tofauti ambayo Diamond anaongozana na Zuchu kuhusu uhusiano wao wa kimapenzi, zimeendelea kushika kasi.


Hii ni baada ya ishara zote kuonesha kuwa, wawili hao sasa ni wapenzi na muda wowote wanatarajia kufunga ndoa. Ukaribu wa Diamond na Zuchu ndiyo uliochochea gumzo na wadadisi wa mambo kuanza kuunganisha nukta ili kupata picha kamili kama ni kweli wawili hao ni wapenzi au la!


Kwa mujibu wa taarifa zilizopo katika makabrasha ya Gazeti la IJUMAA, tangu Lebo ya WCB imchukue Zuchu kama msanii wake, Diamond alikuwa mstari wa mbele katika kumnadi mrembo huyo popote pale anapopata nafasi, iwe kwenye mitandao ya kijamii au kwenye mikutano ya kibiashara anayofanya na kampuni tofauti.


Mfano; Julai 18, 2020 Diamond alitangaza kuwa yupo singo na mashabiki wakae tayari kumuona mrembo wake mpya atakayepita naye kwenye ‘red carpet’ pale Mlimani City kwenye uzinduzi wa albam fupi (EP) ya I Am Zuchu.



Wengine walitarajia Diamond atapita kwenye zulia jekundu na warembo ambao wanafahamika na aliwahi kuwa nao kwenye uhusiano kama vile Zari The Boss Lady, Wema Sepetu, Hamisa Mobeto, Tanasha Donna na wengineo, lakini akawashangaza maahabiki kwa kuingia ukumbini na Zuchu yakiwemo matukio mengi yaliyofuata.

Uhusiano wa Diamond na Zuchu unatajwa kuwa miongoni mwa vipaumbele muhimu kwa mastaa hao ndani ya mwaka huu wa 2022.


BARAKA ZA BI KHADIJA
Januari 31, 2022, mama mzazi wa Zuchu, Khadija Kopa au Bi Khadija alitoa baraka ambazo wadadisi wa mambo wameunganisha taarifa na kupata matokeo kuwa, hizo ni baraka za wawili wapendanao baina ya Diamond na Zuchu.


“Zuhura mwanangu nimekulea kwenye maadili na najua wewe ni binti mwenye maamuzi sahihi na mimi kama Mama yako niseme sina budi kukusapoti.


“Tarehe 14 inaenda kua siku yako kubwa hakuna mwanamke asiye na ndoto hii.Mwenyenzi Mungu akakusimamie najua hutoniangusha.



Siku hii isiwe tu siku yako kubwa duniani basi pia ikawe ndio mwanzo wa maisha mapya yenye furaha. Mwenyenzi Mungu akulinde kiziwanda changu Amin,” aliandika Bi Khadija katika ukurasa wake wa Instargram.


Tukio kubwa linalosubiriwa ni Jumatatu ijayo ambaye ni Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day) ambapo ndipo Zuchu ameahidi kufanya jambo kubwa katika Ukumbi wa Mlimani Citu jijini Dar.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad