Zuchu Apewa Onyo Kali



KWA muda sasa madai yameendelea kusambaa kwamba staa wa muziki barani Afrika, Nasibu Abdul au Diamond Platnumz na msanii wake, Zuhura Othman ‘Zuchu’ wana uhusiano wa kimapenzi.

Ni madai ambayo mtu wa karibu wa familia ya Diamond, Juma Lokole alithibitisha alipozungumza na gazeti hili la IJUMAA.

Juma Lokole anasema kuwa, Diamond na Zuchu wamekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa takriban mwezi mmoja sasa.

“Unajua ukweli mapenzi hayafichiki na ni vizuri tuweke mambo wazi…Zuchu na Diamond wana mahusiano… Hivi sasa ni mwezi mmoja,” anasema Juma lokole.


 
Hivi karibuni, Zuchu alijitokeza hadharani na kumshukuru mpenzi wake ambaye jina lake hakuliweka wazi kwa kumnunulia mdoli mkubwa.

Ikumbukwe mwezi uliopita, Diamond na Zuchu walionekana pamoja usiku kwenye hoteli moja ya kifahari jiji Dar.

Hata hivyo, baadhi ya watu wa karibu na msahabiki wa Zuchu wameendelea kumpa onyo zito, huku wengi wakimwambia kwamba kama hatasikia anachoambiwa, basi ajiandae kujuta.


Doreen Mukami: Sasa hii fisi inataka kuharibia haka kasichana maisha…. Zuchu unafikiria wewe ndiye mzuri au mrembo kuliko hao baby mamas wengine?

Melodious Karani: Diamond baba yao kila msichana poooh…

Musa Yusuph: Zao mbwembwe tuuu na hawadumishi mapenzi yao.

Kitutus Dota: Shida yenu ni hii, hamuwezi kuacha mtu atumie manhood yake kwa amani mpaka mumfatilie…


 
Mercy Mulanda: Mimba loading, huyu huwa halazi damu.

Carl Khivan: Sasa tunangoja mimba na mtoto mwingine, Diamond naye ni nani?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad