Zungu "Staili Yangu ni 'Jaza Ujazwe"




Mgombea wa kiti cha Naibu Spika wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Ilala kupitia tiketi ya CCM, Mussa Azzan Zungu ameomba kupigiwa kura ya NDIYO na wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzani ili kushika nafasi hiyo.




Zungu ambaye ni mgombea pekee wa Unaibu Spika baada ya kutokuwa na Mgombea mwingine kutoka vyama vingine vya upinzani amesema atakapopata nafasi hiyo atafuata maelekezo yote ya Spika kwa mujibu wa kanuni za Bunge.




“Mbali na kufuata maelekezo ya Spika kama Kiongozi wangu, nitahakikisha kusimamia fedha zote zinazopitishwa na Bunge kwenda kwenye miradi mbalimbali ya Maendeleo ya Wananchi zinatumika ipasavyo. Staili yangu ya uongozi ni jaza ujazwe,” amesema Zungu.

Hatua ya uchaguzi huo imekuja kufuatia aliyekuwa naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson kuchaguliwa kuwa Spika baada ya aliyekuwa Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai kujiuzulu.




Zungu ambaye aliingia kwa mbwembwe na kuanza kujinadi kwa Lugha ya Kiingereza aliwaacha wabunge hote hoi kabla ya kubadilisha na kuanza kuongea kwa Lugha ya Kiswahili.

Wabunge 301 waliokuwemo Bungeni wakati wa mchakato huo wamepiga kura ili kumpitisha Zungu kuwa Naibu Spika.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad