Ahmed Ally "Tutachukua kilicho chetu"

Maneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema Uongozi, Wanachama na Mashabiki wa Klabu hiyo hawajakata tamaa na Ubingwa licha ya kuachwa kwa alama 08 katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Young Africans.

Ahmed Ally alitoa kauli hiyo baada ya Simba SC kuifunga Dodoma Jiji FC jana Jumatatu (Machi 07), katika mchezo wa Mzunguuko wa 17 wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Amesema ni mapema mno kwa Simba SC kukubali wameshindwa katika mbio za Ubingwa, kwani hakuna dalili zozote kwa watani zao (Young Africans), kuwapokonya Ubingwa msimu huu.

“Malengo yetu ni kutetea ubingwa wetu wa tano mfululizo, tumepata ushindi wa pili mfululizo tangu tulipoanza mzunguuko wa pili katika Ligi, tukiwa na mabao matano, hii inatuonesha hatujakata tamaa ya kutetea kilicho chetu.”

“Lengo letu ni kushinda kila mchezo ulio mbele yetu, lengo letu ni kushinda michezo 13 iliyosalia katika ligi hii, tunaendelea kupambana ili tuendelee kushinda kila mchezo.”

“Ikifika mzunguuko wa 29 au 30 bado kukiwa na GAPE la alama 08 tutakuja hapa na kusema jamani eeeeh, msimu huu umeisha patupu, tuangalie msimu unaokuja lakini kwa sasa bado tunaendelea kupambana, bado tuna matumaini kwamba muda wowote timu yetu iterejea kwenye ubora wake na hatimaye kukaa kileleni.” amesema Ahmed Ally.

Mabao ya Simba SC katika mchezo huo yamepachikwa wavuni na Clatous Chama kwa mkwaju wa penati na Meddie Kagere.

Ushindi huo unaiwezesha Simba SC kufikisha alama 37 zinazoiweka nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, wakitanguliwa na Young Africans iliyo kileleni kwa alama 45.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad