Akothee Ajuta Kuwaweka Watoto Wake Kwenye Mtanda wa Instagram


Staa wa muziki na mfanyabiashara toka Kenya, mwanamama Akothee ajutia maamuzi yake ya kuwaweka watoto wake mitandaoni.


Mwanamama huyo ambaye jina lake halisi ni Esther Akoth Okeyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameposti chati yake ya mtandao wa WhatsApp (screenshot) na mmoja wa watoto wake ambaye anamuomba afute akaunti yake ya Instagram. “Hili ni kosa ambalo nitaishi nikijutia, kuleta wanangu kwenye mitandao iliyojaa wachawi na uchawi kutoka kona zote za ulimwengu. Mimi nilidhani ni kitu kizuri kuonyesha maisha yangu kama njia ya kutia wengine moyo lakini wapi!” ameandika Akothee.


Aidha, Akothee ametoa ushauri kwa wazazi wengine wasipende kuwaweke watoto wao mitandaoni huku akisema kwamba hili limesababisha aondoe uhusiano wake wa kimapenzi mitandaoni.

“Tayari ninahisi joto na itabidi nitafute njia ya kujisamehe kwa kuumiza familia yangu.” alimalizia Akothee.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad