1: WHAT A PERFOMANCE 🙌 WOW.. JUST WOW 🦁 Pointi 3 za Kibabe.. Mabao 3 ya Kikubwa.. CLEAN SHEET ya heshima kwa KAKOLANYA.. 👏 BINGWA MTETEZI kwenye mawindo yake🦁
2: Well Done Uongozi wa Simba👏 Zile Dakika 45 za kwanza unaelewa kwanini walitumia hela nyingi kuzunguka na CHAMA kule NIGER na MOROCCO bila kumtumia.. Jibu rahisi ni kwamba.. Simba walikuwa wanajiandaa na Ligi wakiwa CAF!
3: Kosa kubwa la Biashara United liko kwenye mkoba wa mbinu wa kocha Vivier Bahati.. Alifeli kwenye mpango, akafeli kwenye uchaguzi wa wachezaji.. Mwisho akafeli kiwanjani. Kivipi?
4: Biashara walianza na Mfumo wa 3-4-3 wakichagua kukabia kwenye mstari wa kati .. Sijui ni mara ngapi walitrain mfumo huu kwenye uwanja wa mazoezi Lakini kurisk situation za 1v1 dhidi ya 'Quality' ya Simba ni kujiwekea ncha ya kisu kwenye koo!
5: 'Poor Selection' ya wachezaji. Baadhi ya wachezaji hawana uzoefu wa kutosha. Sijui ni ipi shida kwa Kisu na Mpapi Nasibu Lakini nafikiri walitakiwa kuwa uwanjani mapema. Uzoefu wao dhidi ya Simba na Uwanja wa Mkapa ungeweza kuwasaidia
6: Kwanini Simba walipunguza kasi kipindi cha pili? Rudi kacheki ratiba inayofata! Kwa uchovu wa safari, bila shaka Pablo alilenga kuumaliza mchezo mapema.. Na akafanikiwa. SHOT ON TARGET 3 za kwanza zikazaa Mabao 3 .. MPANGO SAHIHI🙌
7: SAKHO kulia.. BANDA kushoto.. Kasi yao, Ubora wao wa kukukota na kucheza na mpira bila shaka ni njozi inayotisha kwa mabeki wa pembeni. Hapa unatamani kiungo wa chini awe sharp kwenye kutoa msaada pembeni.. Ukifanya hivyo, unanasa kwenye mtego mwingine.. Upi?
8: CHAMA.. Fundi wa Mpira🙌 Utulivu wake kwenye Zone ya 14! Uharaka wa kufikiri na kufanya maamuzi sahihi ukiruhusu kumpa nafasi, umekwisha
9: Morrison alikuja wakati sahihi kwanjani Lakini sikuelewa kwanini alikuwa hatoa pasi sahihi kwa wenzake.. Movement nyingi za Banda upande wa kulia zilihitaji sana huduma yake na hakuzitoa..
10: Yule Ambrose Awio mtu. Mafie ameonyesha thamani yake.. Bado Israel Patrick anaendelea kutengeneza 'gape' kubwa la ubora kati yake na Kapombe
Nb: Daktari wa Mpira ni Chama tu.. Yule mwingine ni 'Dokta manyau nyau' 😃