Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona Yanga Vs KMC"



1: Kuanzia burudani ya Wasanii, Kwaheri ya Aisha Masaka, Bao la 'kideo la Hersi' na Ubora wa Mayele.. 🙌 Bila shaka YANGA imempa Rais Samia zawadi nzuri ya kujivunia kesho Ofisini

2: 'Creativity Department' ya Yanga inahitaji heshima kubwa 🙌 Nafikiri kwa miaka ya hivi karibuni Yanga ni miongoni mwa TAASISI TATU Bora nchini zinazoweza kuandaa Tukio kubwa la Likavutia kwenye Mtirirko wake✊

3: Zilikuwa Dakika 90 zilizotofautishwa na Ubora wa wachezaji. Tactically, KMC walikuwa na mpango mzuri wa kucheza na Yanga, walichozidiwa ni kumkosa MAYELE kwenye kikosi chao. Kivipi?

4: Kipindi cha kwanza KMC walitengeneza nafasi nyingi.. Za wazi. Ilihitaji utulivu wa mastraika wao kuiumiza Yanga.. Kwa Yanga walihitaji 'Nusu Nafasi', Mayele kuwapa Bao la kuongoza

5: SURE BOY🙌 Amesambaza sana Upendo! Unaweza kudhani ni kazi rahisi kwa kumtazama kwa mbali Lakini ukiangalia Viungo aliopambana nao, utabaini namna ilivyo ngumu kumiliki mchezo dhidi yao

6: Safu ya Ulinzi ya KMC ni kama ilicheza na presha kubwa sana. Bahati mbaya wakaikosa pia 'sauti ya kiongozi' kutoka kwa Kaseja. Ni kama Kaseja alikuwa akipambana na maswali yake kichwani kuhusu mabao aliyofungwa

7: MAYELE🙌 Ni 'Dante' kajifunga! Lakini unahitaji straika mwenye kunusa hatari kwenye boksi kama Mayele ili uone matatizo kwa Dante. What A Player

8: DIARRA! Moja ya mechi nzuri sana akiwa Tanzania. Ni nadra sana kuikuta Yanga ikishambuliwa sana KWA MKAPA! Na Leo Diarra aliamua kuwakumbusha watu kwanini aliitwa 'Mdaka Mishale'

9: Napenda kujitolea kwa Farid Mussa Lakini sidhani kama Yanga wanatakiwa kuendelea 'Kubet' kumpanga Farid kama Beki wa kushoto. Sio kila winga ataamka kama Kipwagile. Ni vyema wakaanza kuwaamini kina YASSIN MUSTAFA kwenye Eneo lao

10: Yanick Bangala✊ What A Player! Nimevutiwa pia na uwezo wa Mvuyekure! Ni kama Miraj Athumani alitakiwa kuwa kwenye mpango wa kwanza wa Hitimana

Nb: Wakirudi wagombee Nafasi ya 2 tu 😃

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad