Aliyekuwa Mke wa Bill Gates Afunguka "Bill gates Alikuwa Anachepuka Nilikuwa Nalia Kila Siku"


Melinda amesema hajilaumu kupasukiana kwa ndoa yake na bilionea Bill Gates kwani alitimiza wajibu wake kama mke na ilifikia hatua ya maumivu akawa hana jinsi ya kuendelea kung'ang'ania ili aonekane bado yupo kwenye ndoa

Bill Gates na Melinda waliachana rasmi mwaka jana baada ya ndoa yao kudumu kwa miaka 27. Katika interview yake ya karibuni tangu kumomonyokeana kwa ndoa hiyo, Melinda ameweka wazi kuwa hajilaumu kwa ndoa yake kubomoka kwani alitimiza wajibu wake tangu walipochumbiana, kuwa ndani ya ndoa na hata alipoamua sasa inatosha akachomoka

Melinda amesema mara kadhaa alikuwa akilia kwani hakuwahi kudhani siku moja ndoa yao itaishia kwa kupeana talaka, huku akimlipua Bill Gates kuwa aliisaliti ndoa yao kwa kuchepuka mara kadhaa ambapo uchepukaji wa Bill Gates na mfanyakazi wa kampuni ya Microsoft uliotokea mwaka 2000 ndio ulioanza kuvunja uaminifu katika ndoa yao

Melinda amesema yeye anaamini katika msamaha na kusamehe na walishajaribu kukaa ili kuyamaliza ili ndoa yao iendelee kuwepo lakini ilifikia hatua ndoa ikawa haina afya tena wala sababu ya kuendelea kung'ang'ania aonekane bado yupo kwenye ndoa

Melinda ameongeza kwamba, kukosa uaminifu kunapotokea mara ya kwanza baina ya wanandoa huwa ngumu sana tena sana kurudisha mambo yawe sawa kama ilivyokuwa mwanzoni

Ameendelea, baada ya kupeana talaka kwasasa yeye na Bill Gates sio marafiki ila wana ukaribu na bado wanashirikiana vizuri tu kikazi na wataendelea kushirikiana vizuri kikazi kwani hata wakati hatua za talaka yao zinaendelea kuna wakati Melinda alikuwa analia kisha masaa kadhaa baadaye wanaweza kuwa pamoja kikazi

Melinda amesema yeye na Bill Gates walijua suala la talaka likiwa hadharani litawashangaza watu na ndivyo ilivyotokea ila amesema hakudhani suala lao la talaka lingekuwa issue kubwa

Kwa ujumla Melinda anasema kuvunjika kwa ndoa yao Bill Gates ndie amechangia sana hilo. Pia amesema maswali mengine kuhusu kilichotokea anapaswa kuulizwa Bill Gates yeye ndie atakuwa na majibu mazuri zaidi

Aidha, Melinda amesema pamoja na yote hawezi kusita kujitosa tena kwenye mahusiano pale atakapoona panamfaa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad