Jeshi la Polisi mkoa wa Kagera linamshikilia mwanaume mmoja Furaha Hansy mwenye umri wa miaka 58 mzaliwa wa Mbeya kwa tuhuma za kupatikana na funguo bandia 97, zikiwamo funguo nne zinazoweza kufungua mlango wowote wa gari, nyumba na pikipiki.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi mkoani Kagera Wankyo Nyegisa, amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Machi 07 mwaka huu akiwa katika nyumba moja ya kulala wageni, katika eneo la Kagabiro wilayani Muleba, na kwamba alipohojiwa amekiri kuhusika na uvunjaji wa nyumba katika mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya na Kagera.