Amuua Mtoto Wake wa Umri wa Wiki Moja Kwa Risasi Tano Kisa Kazaliwa wa Kike


Unyama ! Shahzaib Khan mwanaume wa nchini Pakistani ametiwa mbaroni na polisi kwa kutajwa kumuua mwanae wa kike mwenye umri wa wiki moja, amemuua kwa kumpiga risasi tano. Sababu ya kumuua imeelezwa alitaka mtoto wake wa kwanza kuzaliwa awe wa kiume na sio wa kike

Shahzaib na mkewe wamekuwa kwenye ndoa kwa miaka miwili, baada ya mkewe kujifungua na kusikia kazaa mtoto wa kike, Shahzaib alisita kurudi nyumbani lakini baadaye alirudi na kuwakuta wanafamilia nyumbani. Akamuomba mkewe amkabidhi mtoto ndipo akampiga risasi tano

Ndugu wa kiume upande wa mke amelaani kitendo hicho na kueleza kwamba walipotaka kumdhibiti alikuwa anawatishia na bastola. Alimuua akakimbia hata hivyo alidakwa siku iliyofuata yaani jumanne wiki hii

Mtoto aliyeuliwa alipewa jina la Jannat(Mbingu/pepo)

Suala hilo limeibua hasira miongoni mwa Wapakistani wakitaka mume huyo achukuliwe hatua Kali za kisheria

Nchini Pakistani kwa miongo mingi baadhi ya makabila wanaamini kupata mtoto wa kike ni kama tusi kwa uanaume hivyo baadhi ya wanaharakati nchini humo kukemea imani hizo potofu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad