Meneja Wa Label Ya WCB @babutale Ameweka Wazi Furaha Yake Juu Ya Mafanikio Ya Msanii Wake @rayvanny ambaye Anaendelea Kufanya Mambo Makubwa Kila Siku. Moja Ya Tukio Kubwa ikiwa Ni Kuwa Kwenye List Ya Wasanii Ambao Wanafanya Tour Pamoja Na Msanii Kutoka Columbia MALUMA Ambaye Hadi Sasa Wamefanya Show Kadhaa Kwenye Nchi Kadhaa Jambo Ambalo Kwa Mujibu Wa Tale Ni Moja Ya Kutangaza Muziki Wa Tanzania Nje Ya Mipaka
Tale Amepost Moja Ya Show Aliyofanya Rayvanny Na Maluma Huko Dubai Na Kuandika ✍🏽“MUZIKI WA TANZANIA UNAFUNGUA MILANGO YA DUNIA. Mafanikio yoyote yanatokana na mambo makubwa mawili:
Mosi:Nidhamu ya kazi unayoifanya.
Pili:Kujua malengo yako na malengo ya wanaokuzunguka.
Leo Dunia inashuhuduia Kijana kutoka Mbeya anayefungua milango ya Dunia kwa kupanda mfululizo Majukwaa makubwa yanoyoheshimisha kazi ya Muziki.
Dunia inaandika Historia ya Kijana wa Kiafrika kutoka Familia ya WASAFI (WCB) akishambulia Matamasha makubwa katika pembe tofauti na Ulimwengu akiambatana na Wasanii waliouona uwezo wa Kitanzania.
Haya yote yanaletwa na nidhamu iliyotukuka na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Timu ya usimamizi (Management).
Hongera sana Kijana wangu @rayvanny kwa hatua kubwa ambayo inajiuza yenyewe, hongera Timu nzima ya WASAFI.
Najisikia fahari kuwa sehemu ya Timu inayoshikana nawe mkono usiku na mchana ili kukufanya uzipande vema ngazi za Majukwaa yote ya Muziki Duniani.
Asante Mungu kwa kila hatua, neno "MALENGO"linarudisha tafsiri. MALENGO”