Bajaj Zatumika Ukatili Wa Kingono



JESHI la Polisi mkoani Geita limesema uchunguzi wa awali umebaini pikipiki za matairi matatu (bajaji) zinatumika kutekeleza vitendo vya ukatili wa kingono mjini Geita.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Henry Mwaibambe alisema hayo alipotoa taarifa wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa madereva wa pikipiki za abiria (bodaboda) mjini Geita yaliyoandaliwa na shirika la Plan International.

Kamanda Mwaibambe alisema mwishoni mwa wiki kuwa, zipo taarifa kuwa baadhi ya madereva bajaji wanaofanya safari usiku wanatumia vyombo vyao kufanya ukatili wa kingono ama kusafirisha wasichana wadogo kwenda kufanyiwa vitendo hivo.

"Tumegundua bajaji sasa hivi ni eneo hatarishi kwa mambo ya ukatili wa kingono, watoto wengi wanafanyiwa ukatili kwenye bajaji, au bajaji inatumika kubeba, na tuna baadhi ya kesi tunazo hapa. Wanatumiwa kubeba kwenye bajaji kwenda kufanya ukatili, ndiyo maana tunasema semina hii ya watu wa plan tusiegemee kwa bodaboda peke yao, tuwaeleze hata watu wa bajaji”alisema na kuongeza;

"Hata mambo ya usalama barabarani, sehemu kubwa sasa hivi ni hawa bajaji, bodaboda kidogo tunashukuru Mungu, angalau wameanza kuelewa kidogo, bajaji sasa hivi imekuwa ni shida,"

Aliwaonya madereva bajaji wanaotumika kufanikisha vitendo hivo iwapo watabainika watachukuliwa hatua kali za kisheria kwani kutumika kufanikisha uharifu ni kinyume cha sheria.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad