Balozi wa Uingereza ampongeza Rais Samia





Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, David Concar amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kujieleza.

Hayo ameyasema leo Machi 21, 2022 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Mwanza alipotembelea ofisi za Chama cha waandishi wa habari jijini Mwanza.


Amesema uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kujieleza ni jicho kubwa kwani nchi yake(Uingereza) inapenda kuona suala hilo likitekelezwa.

“Nchi yangu inapenda kuona Tanzania kuna uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kujieleza nila kuwa na vipingamizi kwani ndani ya mwaka mmoja kumekuwa na kuimalika,” amesema Concar.

Aidha, amempongeza Rais Samia kwa kuona umuhimu wa wanawake kwa kufanya uteuzi mbalimbali kwani inaleta hamasa kwenye uongozi wake.

Amesema Uingereza na Tanzania zitaendelea kushirikiana kwenye masuala mbalimbali.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mwanza(MPC), Edwin Soko amesema ni bahati kubwa kwa Tanzania kupata Balozi anayetambua usawa wa kijinsia na ushirikiano mzuri kati ya Tanzania na Uingereza.

Akizungumza kwa niaba ya waandishi wa habari, Flora Magabe amewataka waandishi wa habari kuchangamkia fursa mbalimbali zinajitokea ili kuweza kuongeza maarifa na ujuzi katika shughuli zao.

“Ujio wa balozi umetupa fursa nyingine kuona jinsi tutakapo jadili masuala ya kuaanda maudhui ya usawa wa kijinsia, utawala bora haki za binadamu,”amesema Flora.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad