ASIANZE KAZI: BASATA imemtaka Msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Steve Nyerere asianze kutekeleza majukumu yake hadi hapo itakapoamuliwa na baraza.
Baraza limetoa maelekezo hayo baada ya kikao kilichofanyika leo na sasa linaendelea kufanyia kazi taarifa zilizowasilishwa na shirikisho pamoja na hoja za wajumbe waliohudhuria kikao hicho.