Berkane Walikubali Mziki wa Simba "Simba Itafika Fainali CAF"




KOCHA Mkuu wa RS Berkane ya nchini Morocco, Florent Ibenge, amesifu ubora wa kikosi cha Simba kinachoundwa na nyota kibao, akiwemo Pape Ousmane Sakho raia wa Senegal, huku akiitabiria timu hiyo kufuzu hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.


Kauli hiyo aliitoa mara baada ya mchezo wa nne wa Kombe la Shirikisho Afrika kunako Kundi D, kumalizika kwa Simba kuwafunga Berkane bao 1-0, likifungwa na Sakho, juzi Jumapili.


Akizungumza na Spoti Xtra, Ibenge alisema Simba wameonekana kujiandaa vizuri na michuano hii ambayo malengo yao ni kucheza fainali, hilo linawezekana kutokana na ubora wa kikosi chao msimu huu.


Ibenge alisema katika michuano hii Simba wameonekana kucheza kwa malengo ambayo yamewawezesha kupata matokeo mazuri katika michezo migumu ikiwemo sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya US Gendamerie ya nchini Niger.


“Kitendo cha Simba kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa miaka minne kumewajenga vema, ninaamini katika Shirikisho watafanya vizuri msimu huu.


“Niwatabirie Simba kucheza fainali ya Shirikisho msimu huu kutokana na uzoefu wao walioupata wa ushiriki wa michuano hii mikubwa Afrika kwa miaka minne mfululizo.


“Simba wamejiandaa vizuri, ni wazi inaonesha wana kikosi imara na chenye malengo makubwa, hivyo nilitarajia upinzani tofauti kabla ya kukutana nao katika mchezo huu,” alisema Ibenge

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad