Bibi Mwenye Umri wa Miaka 339 Gumzo Mitandaoni




MAMBO duniani ni mengi aisee! Ni juu yako kuyapembua na kuyaamini au kutokuyaamini.

Hivi; ukiambiwa kuna mzee nchini Uturuki amegonga miaka 339 duniani utaamini?

Basi ishu iko hivyo; ila ukiamini utaungana na wenzako wasioamini na usipoamini utakuwa sehemu ya wasiaomini kwani ndivyo ilivyo kwenye mitandao ya kijamii baada ya video ya mtu huyo kusambaa kwa kasi.



Katika ulimwengu wa mitandao ya kijamii video ya mtu huyo imekuwa agenda, wapo wanaosema haiwezekani mtu akaishi miaka yote hiyo, huku wengine wakisema inawezekana.
Hata hivyo, baada ya video hiyo kuwa gumzo ulimwenguni, jamaa mmoja alijitokeza kwenye mitandao ya kijamii na kujitambuliwa kuwa yeye ni ndugu wa kikongwe huyo na kufafanua kuwa ndugu yake hajafikisha miaka hiyo ila ametimu miaka 109.


 

Katika taarifa yake jamaa huyo aliongeza kuwa, ndugu yake siyo Mturuki bali ni Mthailandi na kutaka watu wamuamini.
Hata hiyo, kama ilivyo mtazamo wa wengi kuhusu video hiyo wapo pia waliopinga ufafanuzi wake huo na kusema jamaa ameutoa bila kuweka vielelezo thabiti na kwamba huenda ameficha taarifa kupunguza “uajabu” wa maisha ya ndugu yake

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad