Ni muendelezo wa Habari za Kimataifa kutokea Bara la Ulaya ambapo tunaangazia mzozo wa Kivita baina ya Ukraine na Urusi.
Licha ya vita hiyo kuwa gumzo Duniani hasa kutokana na misimamo ya Rais wa Urusi Vladimir Putin, huku Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwa anatoa lawama kwa jumuiya mbalimbali yapo mengi yanayojitokez.
Tumeshuhudia Bibi wa miaka 76 akishika Bunduki, tumeshuhudia waliobadilisha jinsia wakizuiwa mipakani, tunashuhudia vifo na athari mbalimbali.
Moja kati ya vitu vilivyowashangaza wengi ni ndoa iliyofungwa na Wanajeshi wakiwa katika uwanja wa Vita.
Unaweza kusema wamekosa uvumilivu lakini ukweli ndio kwamba, Lewis Ivashchenko na Valerii Filimonov wameamua kufunga ndoa katika uwanja wa vita mjini Kyiv.
Itafahamika kwamba Kyiv ni miongoni mwa miji inayotamaniwa na Urusi na umekuwa ukishambuliwa kwa kiasi kikubwa, lakini wawili hao hawakusita kuonyesha hisia zao na kufunga ndoa.
Stori kamili unaweza ukaitazama hii video hapa kufahamu zaidi.