Bilionea Roman Abramovich na Serikali ya Uingereza imeripotiwa wamefikia makubaliano kwa ajili ya suala la mauzo ya timu ya Chelsea.
Serikali inaelezwa kuwa inazingatia suala la timu hiyo kuwekwa sokoni ili kuweza kupata matokeo mazuri kwa ajili ya Chelsea.
Kampuni ya Raine Group imepewa ruhusa ya kuendelea na mchakato wa kusaka mshindani ambaye atachukua timu hiyo.
Hali hiyo imekuja baada ya timu hiyo kuendelea na shughuli zake kama kawaida huku kukiwa na mashaka kuhusu uwezo wa timu hiyo kuweza kumaliza msimu katika hali nzuri.
Kwa mujibu wa The Daily Telegraph, pande zote mbili zipo kwenye mpango wa kuweza kufanya usimamizi mzuri.
Alhamisi iliyopita iliripotiwa kwamba Abramovich alitoa maelekezo ya kusimamisha shughuli zake kutokana na kuhusishwa na ukaribu na Rais Vladimir Putin wa Russia kuhusu kuendelea na mchakato wa kuiweka timu hiyo sokoni, maelekezo hayo inatajwa yalitoka Serikalini.