Bodaboda Yamuwaisha Zuchu Kusaini DILI Alilosotea Miaka Minne



USIKU wa Aprili 8, 2020 WCB Wasafi ilitangaza kumsaini Zuchu ambaye ni mtoto wa Malkia wa Taarabu nchini, Khadija Kopa, lebo hiyo inayomilikiwa na Diamond Platnumz ilikuwa haijamsaini msanii mpya toka Januari 28, 2018 ambapo ilimtambulisha Mbosso.

Sasa ni takribani miaka miwili Zuchu akiwa amejenga picha safi na kubwa katika muziki wake. Ameshatoa EP (I Am Zuchu) na kushinda tuzo (AFRIMMA). Yupo katika safari ya kufikia kilele cha mafanikio yake. Na haya ni mambo 10 wasiyoyafahamu rafiki zako kuhusu Zuchu na muziki wake.

1. Zuchu aliwahi kuwa ‘back vocal artist’ wa Diamond kwa kipindi fulani. Hiyo ni sawa na Bwana Misosi ambaye naye alikuwa akifanya kazi hiyo kwa Profesa Jay kabla ya Chid Benzi na DJ Choka.

2. Anachojivunia Zuchu katika muziki wake ni ‘tone’ yake ya baibuda. Anaamini hii ndio silaha yake inayomtofautisha na wasanii wengine wa kike na ndicho kilimchomvutia Diamond hadi kumsaini WCB.


3. Zuchu alikuwa WCB kwa miaka minne ndipo akatambulishwa kama msanii wao. Wakati lebo inawatoa Lava Lava, Mbosso na kuwatambulisha Rich Mavoko na Queen Darleen, yeye alikuwepo hapo.

4. Mdundo wa wimbo ‘Cheche’ ulitengenezwa na Prodyuza Mocco Genius kwa ajili ya Diamond, Zuchu akauomba na kuurekodia. Diamond alipokuja kusikia alichofanya ndipo akakubali kuingiza ‘verse’ yake. Pia ni wimbo ulioimbwa kwa lugha tatu - Kiswahili, Kiingereza na Kihispaniola.

5. Zuchu ndiye msanii wa kwanza wa kike Tanzania na Afrika Mashariki kufikisha watazamaji (viewers) milioni 100 YouTube, kisha akafuata Nandy ambaye alikuwa naye kwenye mashindano ya Tecno Own The Stage.


6. Siku Zuchu anaenda kusaini mkataba WCB alipanda daladala akaona inamchelewesha. Akashuka akapanda bodaboda hapo alikuwa anatoka ofisi aliyokuwa anaifanyia kazi ambapo siku hiyo aliwaaga wafanyakazi wenzake.

7. Zuchu ndiye msanii wa kwanza wa kike Afrika kufikisha subscribers 100,000 YouTube ndani ya wiki mmoja. Wa kwanza Tanzania kupata followers milioni moja Instagram ndani ya miezi mitano. Wa kwanza Afrika Mashariki kupata subscribers milioni moja YouTube ndani ya mwaka mmoja.

8. Video ya wimbo wa Sukari ndio iliyotazamwa zaidi Afrika kwa mwaka 2021 ikigonga views zaidi milioni 60 YouTube. Hadi sasa inashikilia rekodi kama video ya msanii wa kike Tanzania na Afrika Mashariki kutazamwa zaidi kwa muda wote.

9. Shaa ni miongoni mwa wasanii waliowahi kuandikiwa nyimbo na Zuchu. Hiyo ni sawa na Lady Jaydee aliyewahi kuwaandika wasanii kama Nakaya Sumari, Keisha, Patricia Hillary na Papii Kocha.


10. Zuchu alipokuwa mdogo ndoto yake ilikuwa ni kuwa mwanasheria ila mama’ke, Khadija Kopa ambaye ndiye ‘role model’ wake alitamani afanye muziki. Hata alipotoka masomoni Kopa alimpeleka kwa Babu Tale ili aanza muziki mara moja ila Tale akasema bado mdogo asome.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad