CAF yaipa Simba mashabiki kibao, Ibenge ashtuka



SIMBA wamepata mzuka wa aina yake baada ya Caf kuruhusu kuingiza mashabiki zaidi ya nusu kwenye Uwanja wa Mkapa Jumapili dhidi ya Berkane iliyoanza kuingiwa hofu katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

 Iko hivi, Simba waliomba Shikirikisho la Soka Afrika (Caf) waingize mashabiki 60,000 ili kujaza uwanja katika mchezo wa wikiendi dhidi ya Berkane ya Morocco anakochezea Tuisila Kisinda. Hata hivyo, Caf imewagomea na kuwapa mashabiki 35,000 ambao ni zaidi ya nusu ya uwanja huo unaobeba 60,000.

Itakumbukwa Simba ililala ugenini dhidi ya Wamorocco hao kwa mabao 2-0 matokeo yaliyowaondoa kuongoza kundi D ambalo sasa linaongozwa na Waarabu hao.

Baada ya Simba kushinda juzi dhidi ya Dodoma mzuka wa pili kwao ukawa taarifa hiyo ambapo hesabu zimeanza kuhakikisha wekundu hao wanarudi kuongoza kundi kupitia mchezo huo wa Jumapili kabla ya kuwafuata Asec mchezo utakaopigwa wiki ijayo nchini Benin.


 
Asec inatumia uwanja wa nchini Benin kama wa nyumbani kutokana na uwanja wao kutokidhi viwango huku vile vingine vikifanyiwa ukarabati kwa Fainali za Afrika mwakani.

Meneja mawasiliano wa Simba, Ahmeid Ally ameliambia Mwanaspoti kuwa wanajiandaa kuhakikisha mashabiki hao wanawapa nguvu wachezaji katika mchezo huo.

“Mchezo uliopita tulipewa mashabiki 30,000 lakini inapoongezeka tunatakiwa kuhakikisha Wanasimba na mashabiki wengine watakaokuja wanakuwa na kitu cha kuongeza,”alisema.


Ibenge ashtuka

Taarifa hiyzo za Caf pia Berkane wameiona na haraka mtu wa kwanza kushtuka ni kocha wao Florent Ibenge ambaye ametamka huo ni ugumu mwingine kuelekea mchezo.

Ibenge ameliambia Mwanaspoti kwa simu kuwa anajua nguvu ya mashabiki wa Simba na kwamba hatua hiyo inapaswa kuwa tahadhari kwa wachezaji wake.

“Nimekuwa mzoefu wa kukutana na Simba hapo Tanzania. Nimeona wamepewa mashabiki wa kutosha na mashabiki wao ni watu ambao wanajua kuipa nguvu timu yao, sio tu muda wa mchezo hata kabla ya mchezo, hii ni hatua itakayoongeza ugumu kwetu,” alisema Ibenge ambaye hajawahi kuifunga Simba katika ardhi ya Tanzania tangu akiwa na AS Vita ya kina Djuma Shabaan.

“Nimewaambia wachezaji wangu hautakuwa mchezo rahisi kama ambavyo tulivyoshinda huku Berkane. Tunatakiwa kuwa na utimamu mkubwa wa kujua kucheza mechi ngumu kama hii kama kweli tunataka kufuzu hatua ya robo fainali,” alisema Ibenge ambaye atamuanzisha Tuisila ili kupata sapoti ya mashabiki wa Yanga.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad