Corona Nusura Imuue Paula Uturuki




PAULA Kajala; ni mrembo maarufu Bongo hasa kwenye mitandao ya kijamii ambaye hivi karibu alidaiwa kupata ugonjwa wa Corona au UVIKO-19 akiwa masomoni nchini Uturuki.

 

Inaelezwa kwamba changamoto hiyo nusura imuue Paula ambaye ni binti wa staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja na prodyuza wa muziki nchini Tanzania, P Funk Majani.

 

Mtu wa karibu na familia hiyo aliliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, ugonjwa huo ulikuwa ukimsumbua mno Paula kiasi ambacho mama yake alipitia kipindi kigumu na mara nyingi alikuwa akipandwa na presha kwa kumuwazia mtoto wake huyo ukizingatia alikuwa mbali naye.

 

“Kwa kweli Kajala aliteseka sana tena sana maana Uturuki ni mbali, angewezaje kwenda kwa haraka, lakini mtoto wake huyo alimpa moyo tu kuwa asijali na Mungu atamlinda ndipo Kajala angalau akaweza kula,” anasema mtu huyo.

 

Chanzo hicho kilizidi kuweka wazi kuwa, baada ya Corona kuisha ndipo alipoanza safari ya kurudi nchini Tanzania kwa ajili ya likizo, lakini hata alipofika Bongo bado alikuwa hajapona vizuri.

 

“Unajua Corona inaingia haraka, lakini kutoka ndiyo ngumu hivyo hata alivyokuja huku bado huo ugonjwa unamsumbua sana na anaendelea kuudhibiti kwa sababu wamefunga chuo mpaka mwezi wa nane,” anasema.

 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad