Davido Alimwa Faini ya Bilioni 1 Kuzidisha Dakika 34 Ukumbi wa O2 Arena


Supastaa Davido amejikuta akilimwa kiasi cha £ 340k ambayo ni zaidi ya Bilioni 1 na milioni 46M+ kwa thamani ya pesa ya Tanzania ikiwa ni faini baada ya kuzidisha muda (dakika) katika show yake iliyofanyika mwishoni mwa wikiendi ndani ya ukumbi wa O2 Arena huko London, Uingereza.

Imeripotiwa kuwa, show ya mkali huyo ilipaswa kuisha saa tano kamili usiku ila Davido akatumbuiza hadi saa 5 na dakika 34. Licha ya hayo kujiri, Davido suala hilo alikuwa akilielewa kwani alisema hajali kuhusu faini hiyo.


Fahamu kuwa, utaratibu wa ukumbi wa O2 Arena msanii akizidisha dakika basi anapaswa kulipwa £ 10K. Hivyo kwa Davido na dakika zake 34 ni sawa na £ 340K.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad