Supastaa Davido anazidi kuonyesha jeuri ya fedha, licha ya kuwa na mikoko ya gharama kubwa kwenye eneo la kuegesha magari nyumbani kwake, hilo halimzuii kuongeza mikoko mingine ya gharama.
Mkali huyo ambaye amefanya kwa mafanikio makubwa show yake kwenye ukumbi wa O2 Arena, huko London Uingereza ameripotiwa kununua mkoko mpya aina ya MERCEDEZ MAYBACH GLS 600 ya Mwaka 2022 yenye thamani ya $ 300K ambazo ni takribani Milioni 694 kwa pesa ya Tanzania.
Aidha, katika taarifa nyingine kumuhusu mkali huyo, anatarajia kuipokea Lamborghini yake mpya itue Nigeria kutoka Dubai.