Diamond Platnumz "Nipo Kwenye Penzi Zito"



DIAMOND Platnumz; ni mwanamuziki mkubwa barani Afrika akiiwakilisha vyema nchi yake ya Tanzania ambaye amesisitiza kuwa, yupo kwenye penzi zito.

Diamond au Mondi amedai kwamba, katika penzi alilopo kwa sasa analishwa vinono.

Samba huyo wa Tandale ameendelea kukanusha madai ya kumchumbia msanii wake, Zuchu ambaye yupo chini ya lebo yake ya Wasafi.

“Niko kwenye mahusiano na nina furaha. Ninafurahia mahusiano yangu, yananipa raha na amani, huba limetaradadi,” anasema Diamond wakati huu akiendelea kuitangaza albam yake fupi (EP) ya First Of All (FOA).

Diamond anasema kuwa, anampenda mchumba wake kwa kiasi kuwa anakosa maneno ya kutumia kuelezea hisia zake.

“Nampenda sana naye anafahamu nampenda na maneno tupu hayatoshelezi ila matendo yangu yeye anayaona,” anaongeza Chibu Dangote.

STORI: IJUMAA WIKIENDA, DAR

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad