Supastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amewataka wasanii wenzake wa Bongo kuungana na kuwa kitu kimoja badala ya kugombana na kuchukiana wao kwa wao.
Diamond amesema hayo katika mahojiuano maalum aliyofanya na Wasafi FM wakati akitambulisha EP yake mpya ya FOA.
“Ukienda kweye top yoyote ili ya wasanii Afrika mimi ni namba tatu katika wasanii wakubwa Afrika. Taifa limepeleka mwamba akashindane na watu kwenye mataifa mengine.
“Kufika top 3 kwa wasanii wote afrika sio kitu rahisi, ukigugo hapo utakutana na #Simba bendera ya Tanzania imekaa pale halafu unakuja kunishindanisha na msanii ambaye hata kwenye top 100 hayupo, unanikosea heshima kwanza kuanzia nchi, mashabiki wa nchii hii, familia mpaka watoto zangu.
“Afrika mashariki tuna vipaji sana lakini tunatakiwa tufute yale mawazo ya kushambuliana wenyewe kwa wenyewe, tufikirie kwamba wale wenzatu wanapiga hela tufikirie jinsi ya kushindana nao.
“Kunatakiwa kuwe na wivu wa kimaendeleo unaongeza kasi kwa sababu wale wenzetu wana hasira sana na Dunia lakini unakuta kuna watu wana hasira naDiamond.
“Kuna mentality fulani watanzania lazima tuifute ili we uonekane mkubwa sio lazima ugombane na mtu yani mi sina noma, ila mtu akitaka anivunjie heshima hapo ndo sikubali kila mtu anaheshima yake.
“Ukija kwenye reality nani atafanya vizuri zaidi ndio utaumia hapo kwenye kupendeza, ujue mi ninama-hit, maana nitakupiga kwenye mauzo, kupendeza, nimeachia EP nyimbo zote 10 hit na zingine za kizungu watu wametoa album hapa zimefeli kabisa hamna hata hit moja, album imetoka hamna hata hit moja unaitafuta,” amesema Diamond.