Dk Slaa: Mimi siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa



Mwanza. Balozi Dk Wilbroad Slaa amesema siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa tangu Septemba 1, 2015 alipotangaza kujivua nafasi ya Katibu Mkuu wa Chadema nchini.

Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Machi 25 katika kongamano la kujadili falsafa ya hayati John Magufuli lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) Mwanza huku akiwasisitizia watanzania kutambua hivyo.

Amesema pamoja na kutokuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa nchini ataendelea kutoa maoni na ushauri katika masuala mbalimbali yenye tija kwa taifa.

"Sipo chama chochote lakini niliweka wazi siku najihudhuru kwamba katika masuala ya taifa mimi bado ni mtanzania na nitatoa sauti na kauli yangu katika masuala yanayohusu taifa langu na nitafanya hivyo bila uoga kwani taifa ni la watanzania wote" amesema Dk Slaa


 
Akimzungumzia hayati John Magufuli, Dk Slaa amesema atamkumbuka kiongozi huyo kwa uzalendo aliokuwa nao kwa taifa lake ikiwemo kufuta safari za nje kwa watumishi wa Umma kwa lengo la kupunguza matumizi ya serikali.

Amesema Magufuli pia alisimama kuionyesha na kuiaminisha dunia kwamba Tanzania inaweza kujitegemea kwa kutumia rasilimali ilizonazo na vyanzo vya ndani vya mapato.

"Katika diplomasia ya uchumi, kila tulipokutana Magufuli alisema tuna rasilimali zetu tuwekeze katika hizo ndiyo maana alikuwa hataki kwenda kuomba kama tutaenda basi tunaenda kubadilishana katika mfumo wa usawa hayo ni mapenzi ya dhati aliyekuwa nayo kwa taifa lake," amesema Dk Slaa

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad