DPP awafutia mashtaka ya ugaidi masheikh 15



MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imewaacha huru Masheikh 15, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Sylvester Mwakitalu kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka ya ugaidi yaliyokuwa yanawakabili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Shuraa ya Maimamu, Ibrahim Mkondo, Masheikh hao waliachwa huru, jana tarehe 1 Machi 2022, baada ya kusota mahabusu kwa miaka saba.

“Mkurugenzi wa Mashtaka amewafutia mashtaka ya ugaidi watu 15, jijini Dar es Salaam leo (jana). Katika mashauri hayo ambayo hayakupata kuzungumzwa ndani ya miaka saba, mkurugenzi alitamka mbele ya Jaji kuwa jamhuri haina nia ya kuendelea tena na mashauri hayo,” imesema taarifa ya Mkondo.

Masheikh walioachwa huru ni pamoja na Sheikh Juma Yasin, Ustadhi Abdalla Juma Omar, Nassoro Said Amoor, Ali Nassoro Swala, Juma Zuberi Kitambi, Rajabu Ali Magomba, Hussein Mustafa Juma na Haruna Issa Nkuye.


 
Wengine ni, Buheti Yusuf Buheti, Seif Shaha Jongo, Yusuf Issa Rajab, Hassan Bakari Mnele, Ramia Shaaban Swaleh, Abdul Majid Juma Ludima na Rashid Hassan Mitambo.

Hatua hiyo ni muendelezo wa DPP Mwakitalu kufuta kesi za ugaidi zilizokuwa zinawakabili masheikh waliosota rumande kwa zaidi ya miaka mitano, ambapo hivi karibuni aliwafutia mashtaka masheikh 40.

Masheikh hao 40 walikuwa wanakabiliwa na mashtaka ya ugaidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad