FIFA yazuia mchezo wa Tanzania Vs Botwana



Mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki kati ya Tanzania ‘Taifa Stars’ dhidi ya Botswana ‘The Zebras’ uliokua umepangwa kuchezwa keshokutwa Jumamosi (Machi 26), umefutwa rasmi.

Shirikisho la soka nchini Tanzania ‘TFF’ lilithibitisha uwepo wa mchezo huo kupitia taarifa zililochapishwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za shirikisho hilo, kwa kigezo cha kalenda ya ‘FIFA’.

Hata hivyo taarifa iliyotolewana Chama cha soka nchini Botswana ‘BFA’ imeeleza kuwa mchezo huo umefutwa rasmi kutokana na kanuni na taratibu za ‘FIFA’ zinazotaka nchi mwanachama kucheza michezo miwili ya kirafiki katika kalenda maalum.

“Mchezo wa timu ya taifa ya Botswana uliopangwa kuchezwa dhidi ya Tanzania Machi 26, 2022 umefutwa.”


 
“Mchezo huo umefutwa kutokana na Tanzania kuzialika timu tatu kucheza nazo katika kalenda hii ya ‘FIFA’.”


“Sheria za FIFA zinazosimamia mechi za DARAJA 1 za kimataifa inasema wazi kwamba nchi mwanachama inaruhusiwa kucheza michezo miwili tu kwenye kalenda ya ‘FIFA’.

Tayari Tanzania ‘Taifa Stars’ imeshacheza mchezo mmoja wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati jana Jumatano (Machi 23) na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1, huku ikitarajia kucheza mchezo mwingine dhidi ya Sudani Jumanne (Machi 29), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad