Gari Limewaka...Mastaa SIMBA Waongezewa Mzuka CAF



KATIKA kuhakikisha timu yao inafuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, uongozi wa Simba SC umefanya kikao na wachezaji wote.

Simba ipo nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi D kunako michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, wakiwa na pointi nne, huku RS Berkane ya Morocco ikiwa na sita, ndiyo vinara. Timu hizo Jumapili hii, zinatarajiwa kucheza kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar ukiwa ni mchezo wa nne kila mmoja katika Kundi D.

Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema juzi walifanya kikao na wachezaji, lengo likiwa ni kuwakumbusha majukumu yao ya uwanjani katika kuhakikisha wanachukua pointi zote sita kwenye Uwanja wa Mkapa.


Ally alisema hawataki kuona wanapoteza michezo hiyo miwili watakayocheza uwanja wa nyumbani dhidi ya RS Berkane na US Gendarmarie, huku wakihitaji sare ugenini dhidi ya ASEC Mimosas.


Aliongeza kuwa, wanaamini malengo yao yatatimia katika kufuzu robo fainali ya michuano hiyo inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

“Tunajivunia rekodi nzuri tuliyonayo katika miaka miaka miwili iliyopita tunapocheza uwanja wetu wa nyumbani.

“Rekodi hiyo tumepanga kuiendeleza msimu huu ambao licha ya ugumu, lakini tutahakikisha tunapambana kupata ushindi katika michezo miwili ijayo.


“Tumefanya kikao kizito kikihusisha viongozi na wachezaji ambacho kilikuwa na lengo la kuwaongezea morali na hali ya kujiamini wakiwa uwanjani, pia kuwakumbushia majukumu yao,” alisema Ally.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad