Ghana yafuzu Kombe la DUNIA Ikiitoa Nigeria, Vurugu Kubwa Yatokea na Kusababisha Kifo Cha Mtu Mmoja


 VURUGU kubwa ilitokea usiku wa kuamkia leo kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar kati ya Nigeria dhidi ya Ghana.

Ubao wa Uwanja wa Moshood Abiola nchini Abuja ulisoma Nigeria 1-1 Ghana na Nigeria kuweza kufungashiwa virago kwa Ghana kupata faida ya bao la ugenini na jumla waliweza kufungana bao 1-1.

Baada ya mchezo huo kukamilika mashabiki wa Nigeria maarufu kama Super Eagles walikuwa na hasira kwa timu hiyo kushindwa kufuzu kushiriki Kombe la Dunia tena wakiwa nyumbani waliweza kushuka moja kwa moja eneo la uwanja.

Mashabiki hao walijaribu kuwashambulia wachezaji wa timu ya Taifa ya Ghana na kuharibu baadhi ya miundombinu ya uwanja na kuna video ambayo ilichukuliwa ikionyesha mabomu ya machozi ili kuweza kuwasambaratisha mashabiki hao waliokuwa na hasira kali.

Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Ghana ilikuwa ni sare bila kufungana Uwanja Ohene Djan huko Kumasi na Super Eagels waliamini kwamba itakuwa ni rahisi kwa wao kuweza kufuzu jambo ambalo lilikuwa ni tofauti.

Ghana walianza kufunga kwenye mchezo huo dk ya 10 kupitia kwa Thomas Partey iliwapa nguvu ya kupambana huku lile la Nigeria likifungwa na  nahodha wa Super Eagles William Troost-Ekong ilikuwa dk ya 22.

Afisa wa afya wa shirikisho la soka Afrika CAF, Dr Joseph Kabungo amefariki dunia baada ya kupatwa na shambulio la moyo baada ya kumalizika kwa mchezo baina ya Ghana dhidi ya Nigeria na mashabiki kuingia uwanjani kwenye dimba la Abuja International Stadium

Dr Kabungo ambaye alikuwa msimamizi wa mchezo huo kwenye idara ya afya kutokea CAF, taarifa za awali zinasema alipatwa na umauti kutokana na ugonjwa wa shambulio la moyo pindi mashabiki walipoingia uwanjani baada ya mchezo kumalizika dakika 90   huku shirikisho la soka la Zambia likitoa taarifa kusubiri   ripoti kamili kutoka CAF na FIFA juu ya chanzo cha kifo cha daktari huyo .


“Ni mapema kusema chanzo kilichosababisha kifo cha Dr Kabungo lakini tunasubiri ripoti kamili kutoka CAF na FIFA kuhusu undani wa tukio hilo” amesema Rais FAZ Andrew Kamanga kupitia mtandao wa Twitter


Enzi za uhai wake alidumu kama daktari wa timu ya taifa ya Zambia “Chipolopolo” kuanzia mwaka 2003 mpaka 2016 huku siku za karibuni alichaguliwa kuwa katika kamati ya matabibu ya FIFA  baada ya hapo awali kuwa mjumbe wa kamati ya matabibu wa CAF.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad