H Baba Amgeukia Zuchu "Niambie nitoe Ng'ombe Wangapi Nimuoe"


Msanii wa muziki Bongo, H. Baba ameweka wazi nia yake ya kutaka kumuoa mwimbaji wa WCB Wasafi, Zuchu.

H. Baba amesema yupo tayari kulipa mahari na kutuma wazazi wake waende wakaongee na wazazi wa Zuchu huko Zanzibar.

"Kama nitakubaliwa nikipata bahati hii nitakuwa tayari kumuoa Zuchu, kama mtaniondolea vikwazo nimejipanga nipo tayari niambieni niandae Ng'ombe wangapi au nifanyeje" amesema.

Ameendelea kwa kusema; "Zuchu ni muislam mwenzangu lolote linaweza tokea, acha niandae wazee wangu wakisukuma wakamuone mama pia baba yake kule Zenji, ningependa nimuoe ni binti mstaarabu sana, acha nifate taratibu za kidini".

Ungependa H Baba Amuoe zuchu?

Funguka hapa..


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad