Haji Manara Amuasa Madee "Nasikia Unataka Gombea Ubunge Ila Ukipata Usivamie Vyombo ya Habari na Kusingizia Watu Kesi za Madawa ya Kulevya"



Ameandika Haji Manara:

"Ndugu yangu @madeeali umeamua kuingia kwenye Siasa na nasikia unajiandaa kugombea Ubunge 2025..

Ww ni kijana nataka nikuase kidogo hadharani.

Ikitokea ukapata huo Ubunge na baadae Rais akakufanya uwe na Cheo, please haya yaepuke!!

Kudhulumu watu haki na mali zao,usiwaonee raia kwa kuwabambikizia kesi,usiwe na kiburi cha kutukana walio chini yako,usiwadharau wakubwa wenzio kisa aliyekuteua anakulinda au rafiki yako,

usivamie vyombo vya habari na kuwanyanyasa wamiliki wake kwa maslahi yako,,usithubutu kuwasingizia kesi za madawa ya kulevya watu,na hapa usijaribu kuchafua Watoto wa wakubwa ambao ndio ulikuwa chawa wao.

Usikaribie kujiona wewe ni Mungu Mtu kwa kujiona wewe ndio kila kitu katika dunia hii, kiasi cha kutamka ww ndio Mwanadamu mwenye raha kupita wote ulimwenguni, usikubali tuhuma za kuteka raia,usitishie Viongozi wenzako kwa silaha za moto kwa kuwatuma Askari walio chini yako,,usikwepe kulipa kodi kwa Waziri mwenye mamlaka hyo ,sababu hujui kesho atakuwa nani, usilidharau Bunge na kuliona halina maana,inawezekana kesho ukalihitajia.

Usiwadharau Polisi walio chini ya mwamvuli wako,,kesho wanaweza kuwa mabosi zako, ukifanya hayo tegemea yafuatayo, Cheo kikiondoka utaona dunia chungu,utaona kila mtu anakuonea,utadai mali zisizo zako kinguvu kwa kujisahau kuwa bado wewe ni mkubwa, na ukiikuta Serikali kali kama jina lake utakamatwa kisha utaenda kujibu wapi ulipopata mali zote ulizonazo ilhali mshahara wako wanaujua.

Baadae ntakuasa tena Ndugu yangu wa Damu 🙏🏻"

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad